-->

Friday, January 26, 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI ATEMBELEA USA RIVER NA SAFARI CITY

Ziara ya Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mama Dorothy Mwanyika ambaye ametembelea Miradi ya Safari City na Usa River Satellite City, iliopo katika Jiji la Arusha na kufurahishwa na mpangilio wa miradi yote miwili.
Amehimiza uongozi wa NHC kusimamia miradi hiyo kuhakikisha kwamba matarajio ya wateja katika kuwekeza pesa zao kwa ununuzi wa viwanja na baadaye kujenga nyumba, yanatimia.
Katibu Mkuu akiongozwa na Meneja Mradi kuingia katika ofisi ya Mradi.
Meneja wa Mradi, James Kisarika, akitoa maelezo ya jumla kuhusu maendeleo ya Safari City.
Katibu Mkuu na viongozi wengine akisikiliza mawasilisho kwa makini
Afisa Mipango Miji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Devota Zephrine, akielezea mpangilio wa Mji wa Safari City.
Katibu Mkuu akikagua nyumba za mfano.
Katibu Mkuu akitoa nasaha zake baada ya mawasilisho ya mradi. Alikiri kufurahishwa na mpangilio wa mradi na kuahidi kwamba Wizara ipo pamoja na Shirika katika uendelezaji huu na kwamba wadau kama TARURA washirikishwe pia katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na kushirikisha watumiaji kwa njia ya "road tolls charges".
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu na viongozi aliofuatana nao, kutoka ofisi ya Mkoa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Vitengo vya Ardhi na Usajili wa Hati.